Kuna kitu tunaita "Credibility" hii kitu ikikosekana kwenye Taasisi basi Taasisi inapoteza kuaminika na washirika wake. Mara Nyingi hata kama Taasisi ina matatizo ya ndani lakini ili kulinda hadhi yake kwa washirika wake mara nyingi huwa busara zile tofauti kutofika nje.
Hii ni Mara ya pili Msemaji wa Klabu na Uongozi unatofautiana katika kufikisha Taarifa, Msemaji anatamba kwenye majukwaa kuwa wamemteka mchezaji lakini mwenyekiti wa Bodi anakanusha hakutekwa bali walimaliza Biashara. Aliyeanza kutoa taarifa alipaswa kulindwa.
Maneno mengi ya wasemaji huwa Rasmi jumlisha utani, lakini ukija kukanusha mara mbili au mara Tatu unapelekea Taarifa kutoka kwenye chanzo hicho kutokuaminika. Yaani kiufupi Simba inatufanya tushindwe kuamini nani yupo sahihi kutoa taarifa kutoka kwenye taasisi yao.
Sikuona kama kuna Haja ya hiki alichoongea Mwenyekiti wa Bodi sababu suala lilipita, hapa unamfanya Msemaji aonekane Chale, ilitosha kuliacha hili jambo kwenye Mamlaka za klabu. Kwenye Mawasiliano kuna kitu kinaitwa "Feedback" ambacho hutuambia Taarifa imepokelewaje na Mpokeaji.
Communication Managment ni Somo ambalo wengi wanapaswa kulielewa ili kuepusha mifumo rasmi ya Taasisi kutoa au kukanusha taarifa zilizotoka kwenye taasisi husika hii ni kumlinda mlaji wa Taarifa hizo ili siku zote abaki na imani thabiti. Vinginevyo Walaji hawatoamini Taarifa wataona ukanjanja.