Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yuko wapi Paschal Wawa?

Wawa Paschal Paschal Wawa

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki kisiki wa Simba SC, Paschal Wawa, hajaonekana kwenye michezo ya Simba dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union.

Taharuki hiyo imekuja baada ya Wawa kuonekana kwa mara ya mwisho katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika walipocheza na Jwaneng Glaxy ambapo walipokea kichapo cha 3-1 na kuondolewa katika michuano hiyo.

Katika mchezo huo Beki Wawa alionekana kufanya makosa ambayo inasemekana na wengi ndio yalizalisha magoli mawili ya wapinzani.

Wawa ni beki ambae alikua akipata nafasi ya kuanza katika kila mchezo ndani ya klabu ya simba, sambamba na Onyango alliekuwa akibadilishana na Kennedy Juma.

Baada ya mechi dhidi ya Jwaneng, Simba SC, wamecheza michezo miwili dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union, na beki huyo hajaonekana katika michezo hiyo hata kwa wachezaji wa akiba.

Hakujatoka taarifa yoyote kuonesha kama alikuwa na majeraha ama amekosekana kwa sababu zipi.

Sasa hii leo Mwenyekiti wa Wekundu wa Msimbazi, Murtaza Mangungu, amezungumza kuhusiana na suala hilo.

"Si jambo jema kuulizia mchezaji mmoja mmoja, hii haileti picha nzuri kwa afya ya kikosi"

"Simba haina tatizo na Wawa wala mchezaji yoyote, kwa hiyo kuonekana ama kutoonekana kwa mchezaji mwalimu ndio anaejua, kama ni mgonjwa bila shaka anahudumiwa na timu ya matabibu"

Beki aliyekuwa anacheza na Onyango kwa sasa, Henock Inonga amepewa kadi nyekundu pengine inaweza kuwa nafasi ya Wawa kurudi tena kikosini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live