Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Young Africans yavamia kibabe Mwanza

Young Africans Yavamia Kibabe Mwanza Young Africans yavamia kibabe Mwanza

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: Dar24

Kikosi cha Young Africans kimewasili salama jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold FC utakaopigwa Jumamosi (Oktoba 29).

Miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara itapapatuana katika Uwanja wa CCM Kirumba kuanzia mishale ya saa kumi jioni, huku kila upande ukiwa na hamu ya kuzinasa alama tatu za mchezo huo.

Young Africans ilianza safari ya kuelekea Mwanza mapema leo Alfajiri kwa usafiri wa ndege ikitokea Dar es salaam, huku ikimjumuisha safarini Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernaed Morisson aliyekua akiitumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu.

Afisa Habari wa Young Africans Ally Kamwe alizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza safari ya kuelekea jijini Mwanza, ambapo alisema wanakwenda kupambana na In Shaa Allah wanatarajia alama tatu.

“Lengo na Mipango yetu ni kupambana na kupata alama tatu, tunajua tunakwenda kukutana na timu yenye malengo kama ya kwetu, lakini kwa upande wa Young Africans tumejiandaa kwa ajili ya kuendelea pale tulipoishia, kwenye mchezo wetu dhidi ya KC FC,” alisema Ally Kamwe.

Young Africans inaongoza Msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 17 baada ya kucheza michezo saba, ikifuatiwa na Mtibwa Sugar yenye alama 15 baada ya kucheza michezo minane, huku Simba SC ina alama 14 sawa na Azam FC inayoshika nafasi ya tano.

Chanzo: Dar24