Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Young Africans yaifuata Namungo FC

Mayele Mtwara 1140x640 Young Africans yaifuata Namungo FC

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: Dar24

Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans kimewasili salama mkoani Mtwara tayari wa safari ya kuelekea Lindi ambako kitacheza dhidi ya Namungo FC.

Young Africans itakua mgeni katika mchezo huo wa Mzunguko wa 15 wa Ligi Kuu, ambao umepangwa kuunguruma keshokutwa Jumatano (Desemba 07) katika Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa.

Baada ya kuwasili mkoani Mtwara kikosi cha Young Africans kilipata mapokezi kutoka mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Young Africans imesafiri kuelekea Lindi, saa chache baada ya kucheza mchezo wa Ligi Kuu mzunguko wa 14 dhidi ya Tanzania Prisons jijini Dar es salaam na kuibuka na ushindi wa 1-0, bao ambalo lilifungwa na Kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Ushindi dhidi ya Tanzania Prisons umeifanya Young Africans kufikisha alama 35, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 34, huku Azam FC ikiendelea kuwa na alama 32.

Azam FC itacheza mchezo wake wa 15 leo Jumatatu (Desemba 05) dhidi ya Polisi Tanzania mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro katika Uwanja wa Ushirika.

Chanzo: Dar24