Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Young Africans kushusha mtu kazi

Hersi X Gamondi Usajili Young Africans kushusha mtu kazi

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Young Africans umeweka wazi kuwa utashusha mashine ya maana ndani ya siku saba zijazo, ambapo mchezaji huyo atawashangaza watu wengi huku ukisema mchezaji huyo kila shabiki wa Young Africans anamfahamu kwa kuwa sio mchezaji mgeni kwao.

Baadhi ya wachezaji ambao wanahusishwa kujiunga na Young Africans ni pamoja na Saimon Msuva ambaye kwa sasa amechana na klabu yake ya JS Kabyile ya nchini Algeria ambao wamevunja mkataba wake.

Ofisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema kuwa: “Ndani ya siku saba zijazo taifa litakuwa na mshangao mkubwa sana juu ya usajili ambao tumeufanya, watu watajiuliza huyu mchezaji tuliwezaje kumsajili katika timu yetu.

“Ni mchezaji wa maana ambaye mashabiki wote wa Young Africans wanamfahamu na hata wao pia watashangaa tumefanikiwa vipi kumsajili, lakini sio mashabiki wa Young Africans pekee hata wapinzani wetu pia watajiuliza tumefanikiwa vipi.

“Kwa sasa wacha tuwaambie kuwa ukiachana na mchezaji huyo bado pia kutakuwa na maingizo mengine ambayo kwa taratibu zetu za usajili tunafahamu nini cha kufanya, kwa sasa mashabiki wetu tuwaambie tu kuwa wakae mkao wa kula kwani Rais wetu amefanya balaa jingine kwenye usajili msimu huu,” amesema Kamwe.

Chanzo: Dar24
Related Articles: