Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Young Africans kusajili beki ASEC Mimosas

Image 278.png Young Africans kusajili beki ASEC Mimosas

Sat, 10 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans inatajwa kuwa kwenye mawindo ya saini ya Beki wa kulia kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast, Kouassi Attohoula, ambaye atachukuwa nafasi ya Mamadou Doumbia.

Young Africans inajiandaa kumsajili beki huyo ikiwa ni sehemu ya kukiboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa, ambapo wamedhamiria kufanya makubwa zaidi ya ilivyokuwa msimu huu 2022/23.

Mmoja wa mabosi wa Young Africans amesema kuwa klabu hiyo inakamilisha taratibu za kuipata saini ya beki huyo raia wa Burkina Faso mwenye uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi sambamba na kupiga krosi safi za mabao.

Bosi huyo amesema kuwa, kama dili hilo likikamilika kwa asilimia mia moja, basi upo uwezekano mkubwa wa Doumbia kumpisha Attohoula atakayekuja kucheza nafasi ya beki wa kulia.

Ameongeza kuwa viongozi wa Young Africans wanaangalia uwezekano wa kumtoa kwa mkopo Doumbia katika msimu ujao kwenye timu yake aliyokuwa anaichezea huko nyumbani kwao Mali.

“Kama dili la usajili la Attohoula ambaye ni beki wa Asec Mimosas kutua Young Africans, basi safari ya Doumbia itakuwa imewadia ya kuondolewa ili ampishe huyo beki wa pembeni.

“Attohoula ni kati ya wachezaji walionyesha kiwango bora katika msimu katika Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na Asec Mimosas.

“Na kocha Nabi (Nasreddine) ndiye anayeonekana kuhitaji saini ya Attohoula baada ya kuvutiwa naye baada ya kumuona katika michuano hiyo mikubwa Afrika,” amesema bosi huyo.

Akizungumzia hilo la usajili Nabi amesema: “Usajili wangu utakuwa na baadhi ya maingizo mapya machache katika kikosi changu, nitasajili mabeki wa pembeni, mawinga na washambuliaji kila sehemu wachezaji wawili.”

Chanzo: Dar24