Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Young Africans kung’oa kisiki Tanzania Prisons

Edwin Balua Young Africans kung’oa kisiki Tanzania Prisons

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Klabu ya Young Africans imepiga hodi Tanzania Prisons na kufungua mazungumzo ya kutaka kumsajili Kiungo Mshambuliaji, Edwin Balua anayekipiga katika timu hiyo.

Taarifa zinaeleza kuwa, Young Africans imeanza kufanya vikao na viongozi wa Tanzania Prisons ambayo inamilikiwa na Jeshi la Magereza kwa ajili ya kukamilisha usajili wa kiungo huyo.

Mtoa taarifa huyo amesema kama mazungumzo yatakwenda vizuri, basi kiungo huyo atajiunga na Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili.

Ameongeza kuwa, lengo la kumsajili kiungo huyo ni kuwapunguza wachezaji wengine wazawa waanaocheza nafasi hiyo, ambao wameshindwa kuonesha upinzani.

“Kama muafaka utafikia sehemu nzuri kati ya viongozi wa Tanzania Prisons na Young Africans, basi Balua atajiunga na Young Africans.

Vikao vinaendelea vya viongozi wa timu hizi mbili kwa maana ya Young Africans na Tanzania Prisons, ninaamini vitafikia muafaka mzuri.

“Baada ya mazungumzo hayo kukamilika na kufikia muafaka, basi kila kitu kitawekwa wazi kuhusiana na hatima ya kiungo huyo,” amesema mtoa taarifa huyo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans, Ally Kamwe, hivi karibuni alizungumzia usajili kwa kusema: “Tayari tumemalizana na baadhi ya wachezaji katika usajili wa dirisha dogo, kilichobaki ni kuwatambulisha.”

Chanzo: Dar24
Related Articles: