Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Young Africans SC, The Club Above All

Tano Yanga Young Africans SC, The Club Above All

Fri, 1 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

DAR ES SALAAM YOUNG AFRICANS, mstari wa dharau wanao Barcelona unasema Mes Que Un Club wakimaanisha wao ni zaidi ya klabu, mstari wa kibabe zaidi wanao Real Madrid wao wanajiita Los Galacticos yaani Masupastaa halafu una Mwarabu anaitwa Al Ahly yeye ni Mwananchi kisha una Young Africans ya Mwalimu Nyerere wanajiita The Club Above All, hii ni zaidi ya klabu zote kwenye ardhi hii.

Wahadhiri wa Chuo Kikuu wanasema pressure creates diamonds yani msukumo huzalisha Almas na Wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Ghetto wanasema Heavy is the head that wears the crown, yaani kichwa kizito ndio huvaa kofia ya kifalme! PCM pale Minaki wanasema substitute kote huko waweke Yanga Afrika, alishawahi kufanya balaa Algiers, Kongo, Kusini mwa Afrika na leo ni nyumbani kwake.

Kunayo namna nyingi ya kukubaliana kuwa Yanga Afrika ndio bora kwasasa Ukanda huu wa CECAFA, iwe kwa takwimu, vibao, mitutu ama maridhiano! Mualgeria alipigiwa mpira mpaka akapiga magoti kama kuna namna ya kuepusha na kikombe hiki alichonyweshwa Simba, KMC, Police na wengine basi ingepaswa kuwa hivyo lakini mapenzi ya Mungu ni kuwa aende akasambaze ujumbe kwa mataifa yote kuwa YANGA ni klabu ya mpira.

Alipochukua kichapo Zalan wakasema Sudan hakuna ligi, alipopigwa TP Mazembe wakasema imechoka ile timu, alipopigwa Malumo wakasema imeshuka daraja, alipopigwa KMC wakasema bahasha, mpaka pale ambapo msiba ulipomhusu Simba na sasa CR Belouzdad ambao ni mabingwa mara nne Ligi Kuu Algeria, Football Football! Nani wakumfunga Paka kengele?

Bleach kichwani mpira uwanjani, Stephen Aziz Ki kama Bint wa Kidogo na Heena zake, Pacome Ball Dancer kama Miso Missondo na beat zake, Kennedy Musonda anatembea na P2 siku za hatari anakuja kwenye uokozi, Mudathir Yahya kama Soggy Doggy wa Kibanda cha simu ukibeep yeye anatwanga tu! Joseph Guede naona anapanda taratibu bila haraka kama NGENYE.

Ukiachana na Tanesco, Yanga Afrika ndio tatizo lingine nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live