Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yoro afunga safari kwenda Man United

Leny Yoro Leny Yoro

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United inafanya mazungumzo na wawakilishi wa beki kisiki wa Lille na timu ya taifa ya Ufaransa, Leny Yoro katika dirisha hili la usajili baada ya kufikia makubaliano na timu yake ambayo itailipa Pauni 52 milioni kama ada ya uhamisho.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 18, mkataba wake unatarajiwa kumalizika ifikapo 2025, lakini mwenyewe anadaiwa kuripotiwa kutamani zaidi kutua Real Madrid, lingawa timu hiyo haitaki kutoa kiasi cha pesa kinachohitajika na Lille.

Jana iliripotiwa kuwa beki huyo alifanya safari kwenda England kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho wake katika timu hiyo yenye maskani yake kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Yoro ameonyesha kiwango bora akiwa na kikosi cha kwanza cha Lille kwa msimu uliopita ambapo alicheza mechi 35 za michuano yote.

Nyota huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na washabuliaji katika mipira ya juu, pia amekuwa akiwindwa na timu mbalimbali England, huku pia kukiwa na ofa kadhaa kutoka katika Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga).

ARSENAL inasubiri ofa mbalimbali kutoka Fulham kwa ajili ya kumuuza kiungo wao Emile Smith Rowe baada ya kuikataa ofa ya kwanza kutoka Fulham. Rowe mwenye umri wa miaka 23, ni mmoja kati ya mastaa ambao Arsenal imewaweka sokoni katika dirisha hili ili kupata pesa itakazotumia kufanya usajili wa wachezaji inaowahitaji. Mbali ya Fulham, Crystal Palace pia inamtaka.

MSHAMBULIAJI wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Cole Palmer anatumika kumshawishi straika wa Aston Villa na England, Ollie Watkins akubali kujiunga na Chelsea katika dirisha hili la usajili Ulaya. Watkins ambaye ameonyesha kiwango bora katika michuano ya Euro 2024 iliyomalizika Jumapili iliyopita akiwa na England, mkataba wake unatarajiwa kumalizika itakapofika 2030.

LEICESTER City imewasilisha ofa ya Pauni 21 milioni kwenda Juventus kwa ajili ya kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo, Matias Soule, 21, katika dirisha hili. Hata hivyo, Juventus imekataa ofa hiyo ikisisitiza kwamba inahitaji walau Pauni 25 milioni ili kumuuza staa huyo wa kimataifa wa Argentina. Leicester inajipanga bada ya kurudi kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England msimu ujao.

SOUTHAMPTON imefikia makubaliano na West Ham United kwa ajili ya kumsajili kiungo Flynn Downes, 25, katika dirisha hili na itagharimika kiasi kisichopungua Pauni 18 milioni. Downes ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, katika msimu uliopita alicheza mechi 37 za michuano yote na kufunga mabao mawili na kuna uwezekano akatua kwa miamba hiyo.

TIMU kibao zimeendelea kuonyesha nia ya kutaka kumsajili winga wa Bayern Munich, Mathys Tel katika dirisha hili la majira ya kiangazi lakini mabosi wa Bayern wamesisitiza kwamba hawana mpango wa kumuuza kwa sasa. Inaelezwa kocha mpya Vincent Kompany amewaambia mabosi wa juu wa timu hiyo kwamba Tel ni mmoja kati wachezaji muhimu katika mipango yake kuelekea msimu ujao.

BEKI wa kati wa Fiorentina, Nikola Milenkovic inadawia amewasili England kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha dili la kujiunga na Nottingham Forest katika dirisha hili. Nottingham ilikuwa katika mazungumzo na Fiorentina kwa muda mrefu na sasa kila kitu kipo sawa hivyo staa huyo ameruhusiwa kutua kufanya vipimo vya afya.

MAJADILIANO ya ndani baina ya viongozi wa Fulham yanaendelea ikiwa watume ofa nyingine mpya Manchester United kwa ajili ya kiungo wa timu hiyo Scott McTominay au waachane naye. Awali, Fulham iliwasilisha ofa ya Pauni 17 milioni, lakini ilikataliwa. Timu hiyo inahitaji huduma ya kiungo huyo kuziba pengo la Joao Palhinha aliyejiunga na Bayern.

Chanzo: Mwanaspoti