Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yorke: United inaweza kutwaa ubingwa EPL

Dwight Yorke Man Utd F365 Yorke: United inaweza kutwaa ubingwa EPL

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: Nipashe

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Dwight Yorke, anaamini kikosi hicho chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer kinauwezo wa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England.

Mchezaji huyo wa zamani kutoka Trinidad & Tobago anaamini kikosi cha Man United kimesheheni wachezaji wenye ubora unaoweza kuwafanya kushindana na timu zinazowania ubingwa wa Ligi Kuu England, huku akisisitiza kuwa ina viungo wazuri zaidi ya Liverpool.

“Nadhani tuna wachezaji wanaoweza kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England, je, wanacheza kama mabingwa? Hapana, tukirudi nyuma misimu mitatu au minne wakati Leicester City wanachukua ubingwa, unaweza kuona wachezaji waliokuwa nao na wachezaji tulionao sisi, tuna wachezaji wazuri wanaoweza kuchukua ubingwa,” alisema akinukuliwa na BT Sport.

“Tuna kikosi kizuri, tuna walinzi imara, tuna golikipa bora na washambuliaji hatari, watu wanazungumza kuhusu viungo, huwezi kuwa na timu iliyokamilika.

“Huhitaji kuwa na kikosi kilichokamilika ili uweze kchukua ubingwa, ila unahitaji watu wanaoweza kubadilisha matokeo na kutawala mchezo, tuna Cristiano Ronaldo, Edinson Cavani, Paul Pogba na Raphael Varane ni uwendawazimu kuona nafasi tulipo, ni kweli inavunja moyo kuangalia na ni ngumu kukubali pia.”

Man United watarudi tena uwanjani baada ya mapumziko ya kimataifa na kusafiri kwenda kucheza na Watford Novemba 20, mwaka huu.

Chanzo: Nipashe