Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yondani arejeshwa Stars

Morris Pic 3 Yondani Data Yondani arejeshwa Stars

Sun, 28 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author KOCHA Mkuu wa timu ya Taif 'Taifa Stars' Kim Poulsen amewarejesha kikosini nyota Kelvin Yondani baada ya kukosekana kwa muda mrefu huku akimuita Yohana Mkomola kwa mara ya kwanza.

Poulsen leo Ijumaa Februari 26, 2021 ametangaza kikosi kinachojiandaa kucheza michezo ya kufuzu Afcon dhidi ya Equatorial Guinea na Libya mwezi ujao, Machi.

Yondani alikosekana katika kikosi kilichoshiriki CHAN mwaka huu nchini Cameroon huku akiwa miongoni mwa wachezaji waliofanikisha timu hiyo kufuzu mashindano hayo.

Inaelezwa sababu kubwa ya Yondani kuondolewa katika kikosi hicho ni baada ya kukosa timu alipomaliza mkataba wake na Yanga.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz