Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yericko Nyerere: Simba tulizidiwa kamati

Simba Vs Yanga Aziz Ki Debut.jpeg Simba vs Yanga

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hadi Siku 6 kabla mechi Simba ilikuwa imeushika mchezo vizuri nje ya Uwanja. Kuanzia Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi. Makafara makubwa yalikuwa yamefanyika ipasavyo, na Tulikuwa tumeulinda Uwanja mwanzo mwisho.

Hadi inafika siku moja kabla ya mchezo @simbasctanzania ilikuwa inaongoza 2-0 kwenye ungo wa Mizimu. Ushindi huu wa Simba wa bao 2 siku moja kabla ya game ulikuja baada ya Kamati za Simba kunasa na kuharibu vikosi vya Wachawi wa Yanga vilivyokuwa vimeenda Ngende, Sumbawanga, Kigoma na Zanzibar.

Kukamatwa kwa kamati hizo kuliihakikishia Simba Ushindi, izingatiwe kwamba kwa Wiki nzima Uwanja wa Mkapa ulikuwa umehamishwa na huku pale Taifa pakilindwa kwa nguvu kubwa. Makafala makubwa yalipigwa njia zote atakazopita Yanga kuanzia akitokea Avic Town hadi kufika Uwanja wa Taifa.

Ilipofika saa moja kabla ya mchezo kuanza, ungo ulisoma matokeo 2-1, hali hii ilifanya tuanze uchambuzi kujua yanga wamepataje bao hilo moja ilihali ilikuwa 2 bila. Na hata mpira ulipoanza Yanga wakapata bao, na kisha Simba kusawazisha, Ungo uliendelea kuonyesha matokeo yatakuwa 2-1. Kufumba na kufumbua baada ya mapumziko tu, Hali ilibadilika.

Uchanbuzi wa Kishirikina umekuja kubaini Walituzidi ujanja, Kwanza baada ya kuzikamata zile kamati za uchawi zilizotumwa Ngende, Sumbawanga na Zanzibar, Wenzetu walibadili mbinu haraka wakaenda Mwandoya kwa Mwana Kingi, huko walibadili mbinu siku moja kabla ya mchezo, wakakwepa njia zote tulizotega kuanzia Avic Town, wakati wa kutoka kambini kuja uwanjani walipita Mwasonga, Kibada, Kongowe na kutokea Mbagala tofauti na ilivyozoeleka.

Vita vilikuwa vikubwa Uwanjani, Mwanakingi alifanikiwa kuua njia zote za Kamati ya Simba na ilipofika mapumziko alikuwa amefaulu kupora uwanja na kugeuza kibra na kutuingiza kwenye mfumo. Na hivyo ni wazi pekee Wachawi wa Simba tulizidiwa, Yanga walifanikiwa kuficha magoli, hatukuyaona kabisa.

Tatizo la Simba sio Kocha, ni zaidi ya Kocha. Kamati ya Wazee ijitafakari, Viongozi wa Simba wameshindwa kuwezesha kamati ikafanya kazi yake kwa utulivu. Kuna vifaa tulivihitaji tukashindwa kupata kwasababu ya lugha gongana.

Mwenyekiti wa Simba Mzee Mangungo ni kiunganishi cha Wazee na Klabu, Viongizi wa Simba (Wenye pesa) hawamwezeshi ipasavyo akafanya kazi yake tuliyomtuma wanasimba, Pia na yeye abadilike, amekuwa mzito sana kuchukua hatua. Kishirikina ni wazi Simba tulizidiwa kwa ubora wa mti na tumefungwa nje ya uwanja.

Kwa heri Kocha Bora Afrika Mashariki Na Kati

NJE YA USHIRIKINA.

Simba ina matatizo makubwa yanayoanzia katika bench la ufundi idara ya viungo, Kwakiwango kikubwa Wachezaji hawana utimamu wa miili yao, eneo hili limekuwa tatizo kwa muda mrefu, Kocha wa Viungo ni tatizo kubwa tangu aondoke kocha wa Viungo aliyefanya kazi na Kishingo na Da Rosa.

Pili, lilikuwa kosa kubwa la karne kuwarejesha Friends Of Simba siku tano tu kabla ya mechi na mtani wetu wa jadi, kamati za kazi zilikuwa tayari ziko kazini na zimeshika idara zote, Kitendo cha kuleta kundi lingine lililokuwa nje ya klabu ambalo kiasili huwa linajiitw ndio lenye timu kulipunguza umakini wa maandalizi ya game hii. Ilitakiwa Mo asubiri mpira huu upite ndipo afanye uteuzi wake.

Robertinoh ameondoka, ni kocha mzuri, lakini ni wa daraja dogo ukilinganisha na hadhi ya Simba. Kwa sasa Simba inamhitaji kocha Mkubwa wa hadhi ya Ibenge, Kocha wa TP Mazembe, ama yoyote aliyefundisha timu kubwa inayoshiriki mara nyingi klabu bingwa ngazi ya nusu fainali au faina, sio kocha wa hadhi ya makundi tena.

Tuna michuano ya kimataifa iko mbele yetu, tunahitaji umoja wa hali ya juu sana, Mechi za kimataifa kwetu ni muhimu zaidi, na ifahamike kuwa huwa zinachezwa tofauti kabisa ukilinganisha na mechi za mtani wa jadi. Kanati za ufundi ziimarishwe ipasavyo. Bench la ufundi liimarishwe.

Yericko Nyerere

Chanzo: www.tanzaniaweb.live