Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yao ni Full Package

Yao Yao Jeshi.jpeg Yao kouassi Attohoula

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa masaa machache niliobahatika kumuona Yao kouassi ,Ndani yake nawaona Shadrack Nsajigwa Fuso, Juma Abdul, Godfrey Taita, Fred Mbuna na Shomari Kapombe.

Sina shaka na usajili huu kwa aina ya uchezaji wake, Nilipata kuhudumu nafasi nyingi ikiwemo beki ya kulia,

Kwa uelewa wangu, uzoefu wangu, mafunzo kutoka kwa makocha kwenye nafasi hiyo na pia kwa kuwaona na kucheza pamoja na wachezaji waliofanya/wanaofanya vizuri kwenye nafasi hiyo kama ambavyo nimetangulia kuwataja.

Yao ni mchezaji mwenye hali/attitude lakini anajituma/commitment. Soka ni mchezo wa wazi, soka ni tofauti kidogo na kazi zingine ambazo utendaji wake sio wa wazi sana. Soka halihitaji sana usanii.

Ili uweze kufanya majukumu kwa uweledi ni lazima uwe tayari, na utayari unaanzia kwenye maandalizi/mazoezi husika ya mchezo. Sehemu hii ndio msingi/muongozo wa kile unachoenda kukifanya/apply kwenye mechi.

Yao nimemfuatilia namuona hataki mchezo wakati wa kutekeleza majukumu yake(anajipa deni). Jambo hilo linamfanya kuongeza juhudi na kujituma zaidi. Kwa sifa hii namuona kaka yangu Shadrack Nsajigwa Mwandemele Fuso,

Pia, Yao ni mchezaji anaejua maeneo sahihi wakati wa kushambulia, wapi anatakiwa kuwa timu ikiwa na mpira. Hii inamfanya kushambulia kwenye njia sahihi na wakati sahihi pia. Sifa hii nawaona rafiki zangu Juma Abdul na Shomari Kapombe.

Sambamba na hayo, YAO nimemuona wakati timu haina mpira/timu inashambuliwa. Amekuwa mzuri kuwa kwenye maeneo sahihi lakini pia ana uwezo wa kukaba,

Hapa nawaona kakangu Godfrey Taita na Fred Mbuna. Mabeki wengi sana wa nafasi hii kama sio wote wanakuwa bora ama kwenye kushambulia au kulinda. Wakiwa bora kwenye kushambulia basi wanakuwa si bora katika kujilinda na kinyume chake.

Yaofaida yake nini kwa Kocha? Kocha anapata uhuru wa kumtumia kulingana na mahitaji, aina ya mfumo na aina ya mpinzani pia.

Yao anafaa/fit kwenye matumizi mengi sana kwenye timu, ni kocha tu anahitaji huduma gani kutoka kwake. Deni langu kwake kwa muda mchache niliopata kumuona ni kumwaga maji kama @Juma Abdul kwa Amis Tambwe na Shomari Kapombe kwa John Bocco

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: