Mratibu wa Kikosi cha Young Africans, Hafidh Saleh amesema kuwa beki wao, Attoulah Yao amepona na amefanya mazoezi kamili na kikosi hicho kwa ajili ya mchezo ujao wa ligi dhidi ya watani zao, Simba Sc utakaopigwa Jumamosi, Aprili 20 katika Dimba la Mkapa.
yao aliumiza katika mchezo wa Ligi dhidi ya Azam Fc mwezi Machi ambapo tangu wakati huo amekosa takribani mechi nne za Yanga mpaka sasa akiuguza majeraha yake.
“Beki yao Kuossi Attoula amepona majeraha yake na jana jioni amefanya mazoezi kamili na kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Anaweza kucheza dhidi ya Simba SC Jumamosi kama kocha atataka kumtumia.
“Kuelekea mchezo huo morali ya wachezaji wote iko juu na wamekuwa wakihamasishana kuonesha dhamira yao ya kupata alama tatu keshokutwa Jumamosi (Aprili 20).
"Ni mchezo wachezaji wenyewe wanaoutaka hasa, na mara kwa mara nimewaona wakikumbushana umuhimu wa kushinda mechi hii. Wanataka kuendeleza rekodi ya kuifunga Simba SC msimu huu," amesema Hafidh Saleh.