Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yao aelezea hatma yake Yanga

Yao Pc3 Yao aelezea hatma yake Yanga

Sat, 13 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Yanga, Kouassi Attohoula Yao ameweka wazi bado ana mambo mengi yanayomvutia ndani ya klabu hiyo na hajafikiria kuondoka.

Amesisitiza anachokiona ni katika michuano ya kimataifa msimu ujao watafanya vizuri kuliko msimu huu.

Yao ambae aliumia katika mchezo dhidi ya Azam FC, amekuwa nje kutokana na majeraha, jambo lililomfanya kushindwa kucheza hata mechi za hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa na Yanga ilitolewa kwa mikwaju ya penalti 3-2 dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Tangu kutua katika kikosi hicho msimu huu, amekuwa na uwezo mkubwa jambo lililosababisha kumkalisha benchi Kibwana Shomari, huku akiwa ni beki anaeongoza kwa kuwa asisti sita Ligi Kuu Bara.

Ni miongoni mwa wachezaji watatu tegemeo ambao wote wametoka Ivory Coast katika kikosi cha Asec Mimosas, huku wakitengeneza utatu hatari ndani ya kikosi hicho ambao ni Pacome, yeye mwenyewe na Aziz KI.

Akizungumza na Mwanaspoti alisema licha ya kupata matokeo ambayo hawakuyatarajia katika michuano ya kimataifa, lakini wamefanya kazi kubwa ambayo haiwezi kufutika na wamepata kitu kikubwa watakachokitumia msimu ujao.

Aidha alisema, sasa wamekuwa bora kiakili kwani mechi zilizopita zimetengeneza ujasiri kwa kila mchezaji na kujiona anaweza zaidi ya alivyofikiri na wameonyesha ubora wa hali ya juu ambao hata wapinzani wao wameukubali.

“Baada ya matokeo ya kimataifa naiona Yanga haiko mbali kucheza fainali au kuchukua taji ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao kwani hakuna kinachoshindikana na kinachohitajika ni ubora ambao sisi tunao.

“Nimeridhika na projekti ya Yanga na ninaamini niko sehemu sahihi kutokana na viongozi, benchi la ufundi na mastaa bora ambao wanakufanya ujitume zaidi ili kupata nafasi zaidi,” alisema Yao.

Yanga itacheza na Singida Black Star kiesho jumapili katika uwanja wa CCM Kirumba uliopo Mkoani humo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: