Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yao Yao hatihati kuiokosa Mamelodi

Hatma Ya Majeraha Ya Pacome, Yao Kujulikana Jumatano Yao Yao hatihati kuiokosa Mamelodi

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa pembeni Yao Kouassi ana hatihati kuukosa mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati timu yake ya Yanga SC itakapowavaa mabingwa wa Afrika Kusini, Mamelodi Sandown.

Akitoa taarifa ya majeruhi waliopo kwenye kikosi, Afisa wa Yanga Ali Kamwe amesema, nyota huyo tegemeo kikosini mpaka sasa ana asilimia hamsini kuwepo na hamsini kutokuwepo.

"Yao yeye ni hamsini kwa hamsini, alipata majeraha ya nyama za paja bado anaendelea na matibabu na kwa mujibu wa daktari wetu ni hamsini kwa hamsini kuwepo kwenye mchezo wetu dhidi ya Mamelodi," alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live