Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yao, Farid kuwakosa Kagera Sugar, Aucho hatihati

Yao X Auchoo Yao, Farid kuwakosa Kagera Sugar, Aucho hatihati

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameanika majina ya wachezaji wao ambao watauoksa mchezo dhidi ya Kagera.

Gamondi amesema hayo wakati akizungumza na Yanga TV kuelekea mchezo wa kwanza wa ligi ya NBC dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Alhamisi, Agosti 29, 2024 katika Dimba la Kaitaba Bukoba.

“Yao bado ni majeruhi hatuwezi kuficha hilo, Farid pia ana majeraha makubwa tofauti na tulivyodhani, ana tatizo la majeraha ya misuli ambayo yanaweza kumuweka nje kwa muda mrefu hata miezi miwili. Yeye anapaswa kuamua afanyiwe upasuaji ama lah!

“Mwingine Aucho ambaye anaumwa kidogo lakini amefanya mazoezi vizuri, tutaangalia kama atakuwa fiti tutamtumia lakini wachezaji wengine wote wako fiti kwa ajili ya mchezo huo,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live