Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanick Bangala awashukuru Yanga

Bqngala 958439 Yanick Bangala awashukuru Yanga

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Yannick Bangala amesema haondoki katika klabu ya hiyo kwani anahesmu mkataba wake hadi 2024.

Kauli hiyo ya Bangala inakuja ikiwa ni wiki kadhaa baada ya kuhusishwa kutaka kuondoka klabuni hapo.

"Napenda kuwashukuru mashabiki wote wa Yanga SC kwa sababu siku za hivi karibuni mmeniandika sana kuhusiana na mwenendo wangu katika klabu hii"

"Kama mjuavyo nina mkataba na klabu hii (Yanga SC) mpaka 2024. Na nimepanga kuheshimu mkataba wangu na klabu hii nzuri mpaka mwisho kwa 100%"

"Nimejitoa kufikia matarajio ya timu tukiongozwa na benchi jipya la ufundi, kamati ya utendaji na ninyi mashabiki, kwa sababu bila ninyi hatutaweza kufikia matarajio" amesema Yannick Bangala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live