Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaweka rekodi 6 kali CAF

Yanga ZtR.jpeg Yanga yaweka rekodi 6 kali CAF

Wed, 7 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga imefanikiwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kufanya hivyo.

Pamoja na kwamba imekosa ubingwa baada ya sare ya jumla ya mabao 2-2, lakini Yanga imeweka rekodi kadhaa kubwa Tanzania ambazo hakuna timu nyingine yoyote ambayo imeweza kufanya hivyo kwa miaka mingi.

Michuano ya Shirikisho ni mikubwa kwa bara hili la Afrika ikishika nafasi ya pili baada ya ile ya Ligi ya Mabingwa, ikiwa inatajwa kuwa kati ya mashindano yanayoshirikisha timu nyingi za bara hili.

Yanga hadi wanafika fainali walipita kwenye njia ngumu baada ya kupambana na timu za nchi kubwa kisoka barani Afrika, Club Africain ya Tunisia, TP Mazembe ya Congo, Monastir ya Tunisia, Real Bamako ya Mali, Marumo Gallants ya Afrika Kusini pamoja na US Algier ya Algeria.

Haya ni kati ya mataifa makubwa kwenye soka la Afrika na tayari timu za nchi hizo pamoja na timu zao za taifa zimeshaweka rekodi kadhaa kwenye soka la nchi hii.

Pamoja na kitita cha fedha cha bilioni 2.4 lakini Yanga wamefanikiwaa kuweka rekodi sita kubwa kwa Tanzania jambo ambalo hapo nyuma halikuwahi kutokea:

KUFIKA FAINALI

Yanga imekuwa timu ya kwanza ya Tanzania kufika kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ikiwa inavunja rekodi ya Simba ya kufika hatua ya robo fainali, hii inawafanya kuwa na mzigo mzito kwenye michuano ya msimu ujao, kwani watakuwa wanatakiwa kufanya makubwa kuliko msimu huu au kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

TANZANIA YA 13

Kitendo cha Yanga kufika fainali kimeifanya Tanzania kuwa nchi ya 13 kwenye michuano hii kwa timu yake kufika fainali ya michuano hii kuanzia imeanzishwa mwaka 2014.

Nchi inayoongoza ni Morocco ambayo timu zake zimechukua ubingwa huu mara saba na kushika nafasi ya pili mara mbili, inafuata Tunisia ambayo timu zake zimechukua ubingwa mara tano na kushika nafasi ya pili mara mbili, DR Congo wamefanikiwa kuchukua ubingwa mara mbili na kushika nafasi ya pili mara mbili.

Nyingine ni Misri ambayo timu zake zimetwaa ubingwa mara mbili na kushika nafasi ya pili mara moja, Algeria wametwaa mara moja na kushika nafasi ya pili mara mbili, Ghana wametwaa mara moja na kushika nafasi ya pili mara moja, Mali wametwaa mara moja na nafasi ya pili mara moja, sawa na Congo.

Afrika Kusini wameshika nafasi ya pili mara tatu, nchi za Ivory Coast, Nigeria, Sudan na Tanzania ndiyo pekee ambazo zimefika fainali mara moja lakini hazijatwaa ubingwa.

MABAO 14

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ameweka rekodi ya kuwa mshambuliaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye mashindano ya CAF msimu huu, akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 14.

Achana na mabao saba aliyofunga kwenye michezo ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia hatua ya mtoano, Mayele ambaye pia ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 16, alifanikiwa kufunga mabao sita wakati Yanga walipokutana na Zalan ya Sudan, lakini pia alifunga moja kwenye mchezo ya Ligi ya Mabingwa tena dhidi ya Al Hilal.

YANGA NI TIMU YA 18 AFRIKA

Yanga wameweka rekodi ya kuwa timu ya 28, kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambalo kirekodi linashikiliwa na Club Sfaxien ya Tunisia ambayo imetwaa ubingwa huo mara tatu na kushika nafasi ya pili mara moja.

Wanafuatiwa na Étoile du Sahel ya Tunisia tena ambao wametwaa ubingwa mara mbili, sawa na TP Mazembe, Berkane, Raja Casablanca, timu zilizotwaa mara moja ni tisa zikiongozwa na FAR Rabat, ASM Alger, MAS Fez, AS Léopards, Al Ahly, Zamalek, Hearts of Oak, Stade Malien na FUS Rabat.

Timu 13 zimefika fainali na kushindwa kutwaa ubingwa huo, ikiwemo Yanga kwa nchi majirani, Kenya Tanzania na Uganda, Yanga ndiyo timu pekee iliyofika fainali ya michuano hii.

TIMU YA NNE KUTOLEWA KWA KANUNI

Yanga imekuwa timu ya nne kukosa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na kanuni ya bao la ugenini baada ya mechi kumalizika kwa jumla ya mabao 2-2.

Timu ya kwanza kukosa ubingwa kutokana na kanuni hiyo ni Far Rabat ambao walitoka sare ya jumla ya bao 1-1 na Étoile du Sahel mwaka 2006, nyingine ilitokea mwaka 2008 wakati Club Sfaxien ilipotoka sare ya bao 2-2 na Étoile du Sahel, mwaka 2014, Al Ahly alitwaa ubingwa kwa faida ya bao la ugenini baada ya kupigwa 2-1 na Sewe Sport wakiwa ugenini na alipokwenda nyumbani kwao wakashinda 1-0.

Timu ya nne ni USM Alger ambao wameshinda kwa sare ya mabao 2-2 baada ya kushinda 2-1 Mkapa na kufungwa 1-0 nyumbani kwao.

YANGA YA PILI AFRIKA

Yanga imeweka rekodi ya kuwa timu ya pili kushinda mchezo wa pili wa fainali ikiwa ugenini kwenye dakika tisini baada ya kuwachapa USM bao 1-0, baada ya kulala 2-1 kwenye Uwanja wa Mkapa, lakini ya tatu kwa ujumla baada ya Hearts of Oak kushinda kwa penalti 8-7, dhidi ya Asante Kotoko mwaka 2004.

Hii ni rekodi ambayo imedumu kwa miaka 20, tangu mwaka 2004 michuano hiyo ilipoanza, matokeo ya fainali za pili yalikuwa FAR Rabat 3-0 Dolphins FC, Étoile du Sahel 0–0 FAR Rabat, Club Sfaxien1–0 Al-Merrikh, Étoile du Sahel 2–2 Club Sfaxien, Stade Malien (3–2 p) ES Setif.

Nyingine Club Sfaxien 2–3 FUS de Rabat ikiwa ya kwanza kushinda ugenini mechi ya pili, MAS Fez (6–5 p) Club Africain, AC Léopards 2- 1Djoliba AC, TP Mazembe 2–1 Club Sfaxien, Al Ahly 1–0 Séwé Sport, Étoile du Sahel 1–0 Orlando Pirates, TP Mazembe 4–1 MO Béjaïa.

Pia SuperSport United 0–0 TP Mazembe, AS Vita Club 3–1 Raja CA na Zamalek SC (5–3 p) RS Berkane.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: