Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yawapeleka Waethiopia Zanzibar

Hersi Msigwa Mz Yanga yawapeleka Waethiopia Zanzibar

Sat, 24 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amethibitisha kuwa wameomba mechi yao ya marudiano dhidi ya miamba ya Ethiopia CBE SA ipigwe katika Dimba la Amani Karume, visiwani Zanzibar.

Yanga itaanzia ugenini mechi hiyo ya Raundi ya Kwanza Klabu Bingwa BaraniAfrika, baada ya kuisukuma nje ya Michuano hiyo hatua ya awali Vital'0 ya Burundi kwa Jumla ya Mabao 10-0.

Mechi ya kwanza Yanga ikishinda mabao 4-0 na leo ikikamilisha kalamu ya mabao kwa ushindi wa mabao 6-0.

"Raundi ijayo mchezo wa kwanza tutaanzia ugenini Ethiopia, mchezo wetu wa marudiano tumeomba upigwe Zanzibar. Wananchi wa Dar wamefurahi kwa ushindi wa leo, sasa tunataka tuwapelekee furaha Wananchi wa Zanzibar ili nao wawe sehemu ya kushiriki kampeni yetu ya michuano hii mikubwa Barani Afrika.

"Hii pia ni sehemu ya kuunga miono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya michezo, hivyo tunawaomba mashabiki zetu Zsnzibar na Bara wajiandae, burudani ya raundi inayofuata itakuwa Zanzibar," amesema Eng. Hesri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live