Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yawaita Wananchi Makao Makuu Ijumaa, supu yatajwa

YANGA MASHABIKI ER.jpeg Yanga yawaita Wananchi Makao Makuu Ijumaa hii

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Timu ya Yanga, kinatarajiwa kuanza safari leo kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Yanga na Ahly ambao wote wameshafuzu hatua ya robo fainali, watakipiga kwenye mchezo huo unaotarajiwa kufanyika Ijumaa, Machi 1, 2024 majira ya saa 1:00 nchini Misri.

“Siku ya Ijumaa, Makao Makuu ya Yanga tutafunga ‘big screen’ hapa kwa ajili ya wanachama, mashabiki na wapenzi wa Yanga kujumuika pamoja kuja kufurahia hili jambo na hii tumekuwa tukifanya mara kwa mara timu yetu inapokuwa away.

“Mimi ndiye raia wa shangwe za football, kipigo tulichompa Mwaarabu ninalitafutia namna ya kulinywea supu. Mwarabu kuchukua nne, wanachama watakuja kunywa supu hapa, nafanya mawasiliano na watu wangu wa masoko tujue tunaweza kuangusha ng’ombe wangapi ili Wananchi waje kufurahi tena huku wakiangalia mechi.

“Ninawaalika Wanachama na mashabiki wa Yanga, kuja hapa makao makuu ya yanga kuangalia kwa pamoja mchezo wetu dhidi ya Al Ahly. Tutafanya mawasiliano ya moja kwa moja kwa teknolojia ya kisasa ambapo mtaweza kuwasalimia na kuzungumza na wachezaji na viongozi wakiwa Cairo, mashabiki watawapa ujumbe wachezaji na wachezaji watawapa ahadi mashabiki zao,” amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live