Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yawaingiza chaka CR Belouizdad kiaina

Guede Aziz Ki Yanga yawaingiza chaka CR Belouizdad kiaina

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga imewakwepa kiaina wapinzani wake, CR Belouzidad kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuanzisha kikosi ambacho hakina mastaa wakubwa kwenye mchezo wa Kombe la Shrikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Polisi Tanzania.

Yanga imecheza na Polisi kwenye mchezo wa raundi ya 32 bora ulioanza saa 1:00 jioni jana katika Dimba la Azam Complex, Chamazi huku kikosi kilichotajwa kikiwa bila nyota wake wakubwa.

Kikosi cha Yanga kimeanza bila kipa namba moja, Djigui Diarra mabeki, Dickson Job na Ibrahim Bacca viungo Pacome Zouazou, Maxi Nzegeli pamoja na beki Yao Kouassi wakiwa wamewekwa jukwaani ili kujiandaa kwa mchezo dhidi ya Belouzidad, Jumamosi ijayo.

Hii ina maana kwamba kama wapinzani hao wa Yanga wametuma mashushushu kwenye mchezo huo ili kuitazama timu hiyo inavyocheza, watakuwa wamepotea vibaya kwa kuwa Jumamosi watakutana na watu wengine tofauti.

Kikosi cha Yanga kilichoanza kina mastaa watatu tu ambao wamecheza mechi nyingi msimu huu, Aziz Ki, Joyce Lomarisa na Bakari Mwamnyeto.

Hata hivyo, hii imekuwa mechi ya mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Joseph Guede kuonyesha uwezo wake akiwa ameanza kwenye nafasi ya ushambuliaji na kufungua akaunti ya mabao akifunga mabao mawili kati ya 5-0 ambayo Yanga walishinda katika mchezo huo.

Kikosi kilichoanza cha Yanga kinaongozwa na Abutwalib Mshery, Kibwana Shomary, Joyce Lomalisa, Gift Fred, Bakari Mwamnyeto, Gift Mauya, Agustine Okrah, Jonas Mkude, Aziz Ki na Farid Mussa.

Yanga wanatarajiwa kucheza mechi yao ya marejeano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hata ya makundi dhidi ya CR Belouizdad, Jumamosi ijayo Februari 24, 2024 katika Dimba la Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: