Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yawachimba mkwara Waarabu

Arafat Pic Data Yanga yawachimba mkwara Waarabu

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais Yanga, Arafat Haji ametamba wana kikosi kizuri ambacho kinaweza kushindana na timu kubwa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Arafat alisema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo cha Egyptian Tv kwamba katika mchezo dhidi ya Al Ahly wapo tayari kupambana nao na kuhakikisha wanapata matokeo nyumbani na ugenini lakini watafanya hivyo kwenye michezo mingine ya kundi D.

Arafat alisema wamekuwa wakicheza kwa kujiamini na wanajua wanakutana na timu kubwa kama Al Ahly ambao wanatetea ubingwa, lakini wanaamini kuwa nao wana kikosi kizuri.

“Al Ahly ni timu nzuri na itakuwa inatetea ubingwa. Sisi tunatakiwa kuonyesha kwamba tunastahili kushindana nao na kushinda mechi ya nyumbani na ugenini,” alisema Arafat.

Alisema kama uongozi siku zote wameendelea kulipa benchi la ufundi kila hitaji na wapo tayari kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa.

“Timu yetu ipo tayari kwa Ligi ya Mabingwa. Tuna wachezaji katika timu ya Taifa Tanzania na wapo wachezaji wengine wenye uzoefu wa kutosh. Tunaamini tunaweza kufanya vizuri kwenye michezo yetu ya kundi,” alisema.

Yanga katika kundi la Ligi ya Mabingwa Afrika itaanza kutupa karata yake ya kwanza Novemba 24 dhidi CR Belouizdad ikiwa ugenini nchini Algeria kisha itatupa karata hapa nchini Desemba Mosi kwa kuikaribisha Al Ahly.

Katika kundi Yanga ipo na timu za CR Belouizdad, Medeama na Al Ahly.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live