Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yawaachia Simba kiungo mzambia

Moses Phiri Yanga yawaachia Simba kiungo mzambia

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imefahamika kuwa, uongozi wa Yanga umeachana na mipango ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Zanaco, Mzambia, Moses Phiri na kumuachia kwenda Simba.

Awali Yanga ilikuwa katika mipango ya kumsajili kiungo huyo katika kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano ya kimataifa watakayoshiriki msimu ujao.

Yanga imeanza kukiboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao kwa kuwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji wake.

Kati ya hao ni Kibwana Shomari, Bakari Mwamnyeto na Zawadi Mauya ambao tayari wamesaini sambamba na kutambulishwa.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, amesema kuwa wamejiondoa katika vita hiyo ya kuiwania saini ya Phiri na badala yake kuelekeza mipango yao kwa wachezaji wengine wa kigeni.

Bosi huyo alisema, wameachana na kiungo huyo baada ya kupata taarifa za Simba kumfuata Phiri.

“Rasmi tumewaachia Simba wamsajili Phiri, tumemuondoa katika mipango yetu ya msimu ujao na badala yake nguvu zetu tunazielekeza kwa wachezaji wengine.

“Wapo viungo wengi wenye uwezo mkubwa zaidi ya huyo Phiri, kwa hatua tuliyofikia Yanga siyo ya kugombania wachezaji, kwani wapo wachezaji wengi wazuri na bora.

“Kama tumeweza kutengeneza kikosi bora msimu huu kwa kuwasajili wachezaji wa viwango vya juu tutashindwaje kuwapata kina Aucho (Khalid), Bangala (Yannick), Sure Boy (Salum Aboubakari) na Fei Toto (Feisal Salum Abdallah),” alisema bosi huyo.

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, juzi alizungumzia usajili na kusema: “Moja ya mipango tuliyoiweka katika usajili wa msimu ujao ni kusajili wachezaji wa daraja la juu kabisa.

“Tayari tupo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao wataungana na wenzao katika kutengeneza timu imara ya kubeba makombe ambayo ndiyo kiu kubwa ya Wanayanga.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live