Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yavunja ukimya Aziz Ki kusaini Simba

Aziz KI Yangaaaaaa Yanga yavunja ukimya Aziz Ki kusaini Simba

Mon, 17 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati jina la mfungaji bora ndani ya ligi msimu wa2023/24 Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga likitajwa kuwa kwenye hesabuza watani zao wa jadi Simba, bosi wa Yanga amefungukia ishu hiyo.

Ni mabao 21 Ki alifunga akitoa pasi 8 za mabao na alihusika kwenye mabao29 ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi raia waArgentina.

Gamondi kaongezewa kandarasi ya mwaka mmoja huku Azİz Ki ambayealikuwa ni chaguo la kwanza kwa kocha huyo bado hajaongeza mkataba mpyakuendelea na majukumu yake kwa msimu mpya kwa sasa ni mchezaji huru.

Inaelezwa kuwa kuna timu zaidi ya mbili ambazo zinahitaji saini yake ikiwa niSimba ya Tanzania, Mamelod Sundowns na Kaizer Chiefs za Afrika Kusini.

Kamwe amesema: "Kuna timu nyingi ambazo zinahitaji saini ya Aziz Kitunalitambua ila kuhusu yeye kwenda kwa watani zetu wa jadi, (Simba) labdaatakuwa ni Aziz mweingine ila sio huyu ambaye furaha yake ni ndani ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live