Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yausogelea ubingwa wa NBCPL, yainyuka KMC 1 - 0

Yanga Kmc Fb Yanga yausogelea ubingwa, yampiga 1-0 KMC

Wed, 22 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya YAnga imeendelea kujiweka katika sehemu zuri kutetea taji lake la Ligi Kuu NBC mara baada ya kuinyuka KMC 1-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Yanga Sc iliwapumzisha nyota wao waliocheza kwenye mechi ya Kimataifa akiwemo Mayele, Bangala, Moloko, Job, Lomalisa, Mudathir, Pamoja na Aucho.

Yanga SC ilianza kupata bao dakika ya 38 ya mchezo kupitia kwa nyota wao kinda Clement Mzize ambaye alianza na baadae kumposha Fiston Mayele kipindi cha pili kwenye mchezo huo.

Yanga sasa imefikisha alama 62 ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa imemuacha mpinzani wake Simba SC alama 8 akiwa na alama 54 wote wakiwa wamecheza michezo 23 ikiwa imesalia michezo saba pekee kabla ya Ligi kufika ukingoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live