Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatumia saa 1:30 kuandaa dozi ya Namungo

Mayele1 Kikosi cha Yanga kikifanya mazoezi ya mwisho

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Yanga imetumia saa 1:30 katika mazoezi yao ya mwisho ikijiandaa na mchezo dhidi ya Namungo.

Yanga ilifika uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa saa 2:00 usiku na walifanya mazoezi yao hadi saa 3:30.

Timu hiyo baada ya kufika uwanjani hapa moja kwa moja ilifanya mazoezi mepesi na wengine wakinyooshwa viungo na madaktari wao.

Kocha mkuu wa Yanga, Nassreddine Nabi sambamba na msaidizi wake Cedric Kaze walipanga mipangilio ya mazoezi kisha waliwataka wachezaji wao waende kwenye zoeni la kuruka koni.

Kwenye zoezi hilo walisimamiwa na kocha wa viungo Helmi Gueldich ambaye alikuwa makini muda wote.

Baada ya zoezi hilo Nabi na Kaze waliwataka muda wote wachezaji wao washambulie na kumsimamisha Fiston Mayele sambaba na Aziz Ki kwenye eneo la ushambuliaji.

Ki alipewa maelekezo ya kutosimama kwenye eneo la ushambuliaji badala yake ashuke na kuchukua mipira chini na atakapopata basi aanzie upande wowote wa pembeni.

Mayele alionekana kutokuwa fiti sana lakini mara zote alikuwa anasimama kwenye nafasi (Ndani ya boski) ili aweze kufunga.

Umahiri wa kipa Diara Djigui ulimfanya mshambuliaji huyo asifunge na muda mwingine akipiga mashuti mpira ulikuwa unagonga mwamba. Mwanaspoti. Kata kiu ya mic

Chanzo: Mwanaspoti