Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatuma mkataba kwa Pacha wa Nzengeli

Basiala Pic Basiala Agee

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kilichosalia kwenye dili la winga wa Union Maniema Basiala Agee, labda ni kutua nchini tu, baada ya Yanga kumtumia mkataba haraka ikiwa ni presha ya kocha wao, Miguel Gamondi ambaye ameonekana kuvutiwa naye.

Taarifa za uhakika ambazo Mwanaspoti limejiridhisha ni Yanga imeshatuma mkataba huo na winga huyo atatakiwa kuusaini ndani ya wiki hii na baadaye atatumiwa tiketi ili kuja kujiunga na Wanajangwani hao.

Yanga tayari ilishakubaliana kila kitu na tajiri wa Maniema, Jenerali wa jeshi wa timu hiyo, Amissi Kumba na hatua ya Basiala kusaini sasa inakwenda kuwa uhakika kuwa winga huyo ni mali ya Yanga.

“Yanga wameshatuma mkataba upande wa mchezaji watausoma na kuangalia mambo ya kuweka sawa huku kwa klabu kila kitu kilishamalizika kupitia jenerali (Amissi Kumba),” alisema bosi mmoja wa Maniema.

“Wakimalizana watamtumia tiketi, ili aje lini huko Tanzania, hayo yatakuwa mambo yao kati ya Yanga na mchezaji, wanajua wanafanya njia gani taratibu zao, nafikiri hizi siku mbili Agee atasaini na kuja Tanzania.

Maniema tayari ilishaacha kumtumia Basiala kwenye hesabu zao za msimu huu na kupitia kocha wao, Papy Kimoto ambaye ni staa wa zamani wa nchi hiyo, aliliambia Mwanaspoti alishaanza kupunguza matumizi ya kumtumia winga huyo mara baada ya uongozi wa klabu hiyo kumjulisha watamuuza kwenda Yanga.

Hatua hiyo ya Yanga, Mwanaspoti linafahamu ni presha ya kocha wao Miguel Gamondi ambaye kwenye kila mazungumzo na mabosi wake juu wa timu hiyo hakosi kuuulizia hatua ya usajili wa winga huyo anayeonyesha kiwango cha juu kwa sasa Congo.

Gamondi amewaambia mabosi wake mbali na ujio wa Okrah, bado anamtaka Basiala akitaka kuwa na kikosi chenye sura tofauti katika mechi za mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika zitakazoendelea Februari mwaka huu.

Basiala msimu huu akiwa na Maniema amefunga mabao matano na kutoa asisti tano akiwa mmoja wa mastaa wa muhimu na timu hiyo.

Hata hivyo, chanzo cha ndani ya Yanga kilieleza Mwanaspoti taarifa za mchezaji huyo ni kweli, lakini haifahamika atatua nchini lini kuungana na wenzake.

“Ni kweli dili hilo lipo, anaweza kukamilisha kila kitu hivi karibuni, lakini bado hatujaelezwa atakuja lini hapa nchini, ingawa nafahamu kuwa alishatumiwa mkataba.”

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: