Msafara wa kikosi cha Timu ya Yanga kimetua salama katika Mji wa Bamako nchini Mali majira ya saa 8:40 mchana za nchini humo ambapo ni tofauti ya saa tatu na Tanzania.
Mechi ya Yanga na Real Bamako itachezwa keshokutwa Jumapili, Februari 26, 2023 majira ya saa 1:00 jioni kwa saa za Mali ambapo ni sawa na saa 10:00 kwa saa za Tanzania.
“Tumefikia kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano inayotwa Amitee kwa ajili kuweka kambi yake kujiandaa na mchezo na Real Bamako utakaopigwa Jumapili.
“Leo (jana Alhamisi) tuna program moja tu ya recovery sababu safari ilikuwa ndefu. Kesho (leo Ijumaa) kutakuwa na session moja ya ufundi ambayo itafanyika saa 10:00 jioni kwa saa za mali. Jumamosi pia kutakuwa na session moja, muda ni ule ule wa mchezo kwa ajili ya kuiandaa timu.
“Tunawaomba mashabiki waendelee kuiombea Timu yao ya Yanga ili iendelee kuliwakilisha vizuri Taifa katika mashindano ya kimataifa. Tulichokifanya kwa TP Mazembe, tunaamini tutakifanya tena hapa hapa Bamako Mali, asanteni Wananchi,” amesema Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe.
Yanga wanaenda Mali ???????? kucheza na Real Bamako, katika kikosi cha Yanga kuna Djigui Diarra na Mamadou Doumbia ambao wote ni raia wa Mali, hivyo wataisaidia vyema Yanga, wakienda Dr Congo vs TP MAZEMBE, Yanga pia watakuwa wenyeji huko, kina Yanick Bangala, Fiston Mayele, Tuisila Kisinda, Jesus Moloko na Joyce Lomalisa wapo pia.
Afisa habari wa Young Africans SC Ally Kamwe akiongea na #wananchi kuhusu ratiba ya timu mara baada ya kuwasili nchini Mali.#timuyawananchi #daimambelenyumamwiko pic.twitter.com/EzjjJDbDmR
— Young Africans SC (@yangasc1935) February 23, 2023