Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatua Lindi kuwavaa Namungo

Yanga Wqed Yanga yatua Lindi kuwavaa Namungo

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimewasili salama Ruagwa, Lindi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.

Jana, Desemba 5, 2022 kikosi kilisepa Dar na kuibukia Mtwara kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mchezo huo.

Yanga inatarajiwa kumenyana na Namungo ukiwa ni mchezo wa kufungia mzunguko wa kwanza 2022/23 mpaka sasa ikiwa imecheza mechi 14.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Desemba 7,2022 ambapo Namungo imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Singida Big Stars.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza kibindoni imekusanya pointi 35,mchezo wake uliopita ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-0 Prisons.

Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye msafara huo ni Feisal Salum, Fiston Mayele, Jesus Moloko na Bernard Morrison.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live