Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatoa kauli usajili wa Mahop na Sudi

Sudi Cameroon Yanga yatoa kauli usajili wa Mahop na Sudi

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga kupitia kwa Ofisa habari wake, Ali Kamwe imeweka wazi kuhusu taarifa za usajili na majina yanayohusishwa kusajiliwa na Klabu hiyo huku akisema hawana mpango wowote wa kumsajili mashambuliaji Emmanuel Mahop Dikongue pamoja na Sudi Abdallah.

Kamwe amesema hayo mara baada ya taarifa kusambaa kuwa tayari wameshamalizana na mahop ambaye ni raia wa Cameroon na mfungaji bora wa Ligi Kuu ya nchini humo huku pia Sudi naye ambaye ni raia wa Burundi akitajwa kutua kwa Wananchi.

“Emmanuel hatujawahi kuwa na mpango wake kabisa, Sudi Abdallah pia hayupo kabisa, shida ni kwamba msimu huu Yanga imehusishwa na wachezaji wengi zaidi katika historia ya dirisha la usajili.

“Hawa tunaowaona mitandaoni sijui Sudi, Emmanuel, hapana, hatujawahi kuwa na mpango na hao watu labda ni mawakala tu wanajaribu kupigisha shoti na nimeona wametembea kweli mitandaoni mpaka kwenye magrupu ya Yanga,” amesema Ali Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live