Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatoa burudani Zanzibar

Yanga Zanzibar.jpeg Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo akipambana na mchezaji wa mlandege

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pengine labda watanzania kutoka visiwani walikua wakisikia tu soka la kitabuni linalochezwa na Yanga SC.

Yanga ipo visiwani Zanzibar na usiku wa jana ilikuwa uwanja kukipiga na timu ya Mlandege FC ya visiwani humo.

Bao pekee la mshambuliaji Mkongo, Heritier Ebenezer Makambo dakika ya 50 limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mlandege FC katika mchezo wa kirafiki usiku wa jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Yanga imekwenda Zanzibar kuweka kambi ya wiki moja na siku kadhaa kujiandaa na mechi yake ijayo Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Namungo FC Novemba 20 Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.

Baada ya mchezo wa jana, Yanga iitateremka tena dimbani Novemba 12 kumenyana na KMKM hapo hapo Amaan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live