Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatinga tano bora CAF, Diarra 'out'

Yanga Gamondi Wachezaji Yanga yatinga tano bora CAF, Diarra 'out'

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bado wapo wapo sana tuzo za CAF 2023. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara na washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita Yanga SC ni miongoni mwa timu tano zilizotinga kuwania tuzo ya klabu bora kwa wanaume za CAF kwa mwaka 2023.

Awali zilikuwa zinawania timu 10, Al Ahly ya Misri, Wydad na Raja Casablanca kutoka Morocco, Mamelodi Sundowns na Marumo Gallants kutoka Afrika Kusini, Esperance de Tunisia, USM Alger na CR Belouizdad kutoka Algeria, Asec Mimosa ya Ivory Coast na Tanzania ikiwakilishwa na Yanga SC.

Katika kipengele cha wanaowania tuzo ya kipa bora wa mwaka CAF 2023, kipa wa timu ya taifa ya Mali na Yanga, Djigui Diarra ameshindwa kupenya kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hiyo, huku Mcameroon anayeidakia Manchester United, Andre Onana akitinga tano bora kwenye tuzo hizo za CAF 2023.

Kwenye tuzo hizo Onana anawania na na kipa wa Al Ahly, Mohammed El Shenawy ambaye ndio alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2022, katika orodha hii pia kuna kipa wa Mamelodi Sundown, Ronwen William, Edourd Mendy na Yassine Bounou kutoka Morocco.

Diarra hakuwa na bahati baada ya kutemwa tena tuzo za mchezaji bora wa mashindani CAF huku mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Fiston Mayele ambaye kwa sasa anakipiga Pyramids ya Misri akiburuzana na mastaa tisa katika tuzo hizo.

Mastaa hao ni Percy Tau, Mohammed El Shenawy, Mohmoud Abelmoneim, Ali Maaloul wanaokiwasha Al Ahly, Petter Shalulile wa Mamelodi Sundowns, Yahya Jabrane na Yahya Attiyat Allah kutoka Wydad Casablanca Zineddine Belaid wa USM Alger na Aymen Mahioyus anayekipiga Yverdon Sport akitokea USM Alger.

Tuzo hizo zitatolewa Desemba 11 mwaka huu chini Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live