Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatinga Robo Fainali CRDB Confederation Cup kibabe, yamuua Dodoma 2-0

Mzizeeee Yanga yatinga Robo Fainali CRDB Confederation Cup kibabe, yamuua Dodoma 2-0

Thu, 11 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Magoli mawili yaliyowekwa kambani na Yanga SC yametosha kuiwezesha kuingia hatua ya Robo Fainali katika Kombe la Shirikisho la CRDB hapo jana Aprili 10, 2024.

Mchezo huo dhidi ya wenyeji Dodoma Jiji ulipigwa katika dimba la Jamhuri jijini Dodoma ambapo magoli hayo yalifungwa na Emmanuel Martin wa Dodoma aliyejifunga dakika ya 3 ya mchezo baada ya Agustine Okrah kupiga krosi maridadi golini.

Kipindi cha pili, Dodoma walirudi kwa kushambulia zaidi na kuweza kupata penalti lakini hata hivyo Iddi Kipwagile akaipaisha juu na baadaye Clement Mzize akawaongezea Yanga chuma ya pili iliyowafanya Dodoma wakate tamaa ya kujipapatua hadi mwisho wa mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live