Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatinga Jamhuri kwa miguu

Yanga Jamhuri Morogoro Yanga yatinga Jamhuri kwa miguu

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga imeingia kwenye Uwanja Jamhuri kwa staili ya aina yake ikishuka mbali na geti la kuingilia huku wachezaji wote wakitembea kwa miguu.

Wageni Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kufika Uwanja wa Jamhuri ikitua saa 8:30 kisha basi lao likaishia kwa mbali pembeni kidogo ya geti kubwa baada ya kushindwa kukata Kona katikati ya miti iliyopo pembeni ya Uwanja wa Jamhuri.

Baada ya hapo kikosi kizima cha Yanga kikashuka na kutembea kwa miguu kwenda geti la kuingilia uwanjani wakiongozwa na nahodha wao msaidizi, Dickson Job.

Wakati wote ambao kikosi hicho kikitembea mashabiki wao walionekana kuwashangilia wakifurahia kuwaona mastaa wao vizuri wakiwa wanatembea kuingia ndani ya uwanja.

Baada ya dakika tano baadaye 8:35 wenyeji KMC ilitua uwanjani hapo huku basi lao likisogea hadi karibu na geti la kuingia huku wakikumbana na zomea zomea ya mashabiki wanaodhaniwa ni wa Yanga.

Timu hizo zitapambana kwenye mchezo wa kwanza wa duru la pili unaotarajiwa kuanza saa 10:00 jioni hapa Uwanja wa Jamhuri.

Chanzo: Mwanaspoti