Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatimkia Morogoro kuifuata KMC

Yanga 8 1024x910 Yanga yatimkia Morogoro kuifuata KMC

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya Young Africans SC, leo kimesafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC ambao tutakuwa ugenini.

Mchezo huo wa kwanza katika mzunguko wa pili, unatarajiwa kuchezwa Jumamosi hii ya Februari 17, 2024 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kabla ya kuanza safari hiyo, kikosi kilifika Makao Makuu ya Klabu, Jangwani, Dar es Salaam, ambapo kilifanya ziara fupi na kushuhudia sura mpya ya jengo hilo lililofanyiwa ukarabati mkubwa uliokamilika hivi karibuni.

Katika Ligi Kuu ya NBC, Young Africans SC inaongoza msimamo ikiwa na pointi 40 baada ya kucheza mechi 15.

Ikumbukwe kwamba, mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga ilipocheza dhidi ya KMC, iliibuka na ushindi wa magoli 5-0, tukiwa wenyeji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live