Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yathibitisha Pacome kucheza leo

Lomalisa Pacome Mkudee Pcome, Lomalisa na Mkude

Wed, 1 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua yupo fiti na anatarajiwa kuwepo katika kikosi kitakachocheza mchezo wa leo usiku dhidi ya Tabora United utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Taarifa ya Yanga imeeleza;

Wakati Pacome akirejea, katika mchezo wa leo wa robo fainali ya CRDB Federation Cup tutawakosa Jonas Mkude na Lomalisa Mutambala.

Pacome anarejea uwanjani baada ya kukosekana kwa takribani siku 44 tangu alipoumia Machi 17, mwaka huu.

Kiungo huyo alikosekana kwenye mechi saba za michuano yote ambayo timu yetu ya Young Africans ilicheza ikiwemo miwili ya hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live