Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatangaza sifa za mbadala wa Mwambusi

8a0c70ce67d98e9e21f48ce8a1968f6f Yanga yatangaza sifa za mbadala wa Mwambusi

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU ya Yanga imetangaza vigezo vya mtu atakayechukua mikoba ya kocha msaidizi Juma Mwambusi aliyejiuzulu hivi karibuni, imeelezwa.

Mwambusi aliachia ngazi akitoa sababu ya matatizo ya kiafya.

Kaimu katibu mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema wameanza zoezi la kupitia wasifu (CV) za makocha mbalimbali walioomba kazi, ambapo jopo hilo linaongozwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

“ Mchakato utachukua muda mrefu kidogo, na nikuambia tu tumeanza kupitia wasifu wa baadhi ya makocha ambao wameomba kazi, lakini kikubwa tunahitaji kupata mtu atakayekuja kuongeza kitu cha ziada kwenye benchi letu,”alisema Mfikirwa.

Akitangaza sifa za kocha anayetakiwa kuchukua nafasi hiyo ni kwanza awe Mtanzania ili kurahisisha kazi katika utendaji wa benchi hilo al ufundi.

Alisema wapo makini na wanajitahidi kusimamia vigezo walivyoweka kwakuwa malengo yao ni kuona wanafanya vyema kwenye michezo iliyosalia ya mzunguko wa pili Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mfikirwa amewaomba wanachama na mashabiki kuwa na subra kwatika kipindi hiki ambacho wanafanya kila jitihada kuona wanatimiza jukumu la kumpata msaidi wa Kaze kwa wakati.

Yanga wanaongoza ligi wakiwa na pointi 44, baada ya kucheza michezo 18 huku wakishinda mechi 13, sare tano huku wakishikilia rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi hiyo tangu ilipoanza Septemba 6, 2020.

Chanzo: habarileo.co.tz