Uongozi wa Klabu ya Yanga umetangaza kuacahana na aliyekuwa Mkurugenzi wao wa Matawi na Wanachama, CPA Haji Mfikirwa baada ya kumaliza mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo ya Wananchi.
Ajira ya Mfikirwa imekoma rasmi jana baada ya kutaarifiwa kuondolewa kwenye nafasi yake kufuatia kile kilichoelezwa kutofautiana na uongozi wa klabu hiyo juu ya utekelezaji wa majukumu yake.
CPA Haji Mfikirwa alikuwa amesimamishwa kwa miezi mitatu hivyo klabu imefikia uamuzi wa kuachana nae, huku nafasi hiyo kwa sasa ikiwa wazi na klabu inaendelea na mchakato wa kumsaka Mrithi wake.
Baadhi ya sababu zinatajwa kuwa ni kusuasua kwa zoezi la uandikishaji wa Mashabiki na Wanachama wapya wa klabu hiyo, ikumbukwe CPA Mfikirwa awali alikuwa Mkurugenzi wa Fedha ndani ya makutano ya Twiga na Jangwani.
Nani avae viatu vyake hapo Jangwani?