Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatangaza Jumamosi ni 'Pacome Day'

Pacome Yanga Al Ahly.jpeg Yanga yatangaza Jumamosi ni 'Pacome Day'

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imeendelea na utaratibu wake wa kuzipa mechi zao za nyumbani kwenye michuano ya CAFCL majina ya wachezaji wao kwa ajili ya kuongeza hamasa kwa wachezaji na mashabiki ili waweze kujitokeza na kufanya vizuri katika michezo hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati akitangaza uzinduzi wa hamasa kuelekea mchezo wao wa marejeano dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria utakaopigwa Jumamosi ijayo Februari 24, 2024 katika Dimba la Mkapa na kuupa mchezo huo jina la 'Pacome Day Kitaalam Zaidi'.

"Tulikaa na uongozi, benchi la ufundi na wachezaji, tukatazama umuhimu wa mchezo husika ili kutengeneza hamasa na ari ya timu, tukakubaliana mtoko wetu Jumamosi kwenye mechi dhidi ya Belouizdad iwe ‘Pacome Day Kitaalam Zaidi’.

"Wanayanga ambao mpo tayari kupiga bleach mje mkiwa mmepiga bleach, mimi mwenyewe sijanyoa nwele zangu, nitapiga bleach, kama unataka kupiga bleach kwenye ndevu ruksa na maeneo mengine.

"Kama huwezi kuweka bleach kichwani au kwenye ndevu basi unaweza kuchora mchoro shavuni, kwenye uso, mkononi au popote, ukitaka kuandika jina la Yanga andika, jina la pacome au namba yake ya jezi. Kina dada mnaofuga kucha chora ‘Kipacome’ kucha zako zipendeze.

"GSM amesema hatoiacha siku hii ipite hivi hivi, litatengenezwa eneo maalum la ‘Fans Zone’, shabiki yoyote ukipita pale umependeza, utapewa zawadi yako. Ipo package maalum itakayotolewa kwa shabiki atakayetokelezea vizuri zaidi. GSM hatoi diary na pen.

"Hii ndiyo timu yenye furaha zaidi Afrika, kwa hiyo Jumamosi itakuwa siku yetu ya furaha WanaYanga, kama alivyotufunga kwao, lazima Mwarabu tumkande kwa Mkapa, sisi hatuna mambo ya unyonge wala hatutaki kuwa wanyonge," amesema Ahmed Ally.

Ikumbukwe kuwa, Yanga ilishawahi kutambulisha Maxi Day, Aziz Ki Day, Bacca Day, lengo likiwa ni kuongeza hamasa kuelekea michezo yao ya kimataifa.

Je, upo tayari kupata Bleach siku hiyo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live