Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatamba kubeba makombe yote tena msimu huu

Maxresdefault 8 Yanga yatamba kubeba makombe yote tena msimu huu

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndani ya Yanga kwa sasa ni raha na vicheko tu kutokana na fedha ambazo zinaendelea kuingia kwenye timu hiyo kupitia wadhamini ambapo mabosi wa timu hiyo mapema tu wametamba wanataka kubeba mataji yote kama msimu uliopita.

Mabosi hao wameongeza kuwa wanataka kubeba mataji yao yote waliyotwaa msimu uliopita ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam Sports ikiwa ni mkakati wao wa kutawala soka la Tanzania.

Kauli hiyo ya kibabe inakuja baada ya timu hiyo wiki hii kusaini mkataba wa udhamini na Kampuni ya SportPesa wa bilioni 12.3 huku wakiwa na uhakika wa kuingiza zaidi ya bilioni moja kwa mwezi ukiunganisha fedha za wadhamini wao wote.

Kikosi hicho kwa sasa kinaendelea na maandalizi yake kule Avic Town, Kigamboni wakiwa wanajiandaa na msimu mpya wa ligi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Abbas Tarimba alisema: “Tunajivunia kwa kufanikisha tukio letu muhimu la uzinduzi wa jezi mpya ambazo bila shaka yoyote ndizo jezi bora zaidi kuiwahi kutengenezwa nasi, hii ni sehemu ya maandalizi yetu ya kabla ya msimu.

“Matarajio ni makubwa kwa msimu ujao na kwa namna ninavyoona mipango inayoendelea kuwekwa hususani katika kuboresha nguvu ya uchumi, basi msimu ujao naiona Yanga ikishinda tena mataji yote matatu na kufanya mambo makubwa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live