Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yasuka kikosi kazi, yamrejesha mbaya wa Simba

Yanga Pacome X Kibabage Yanga yasuka kikosi kazi, yamrejesha mbaya wa Simba

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Yanga kwa kundi la pili limepaa leo kuifuata CBE SA ya Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kabla ya kung’oa Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said akaunda jeshi jipya la kikosi kazi chenye sura za rekodi.

Hersi ameunda kamati mpya ya mashindano yenye watu nane akiendelea kumuamini Rodgers Gumbo aliyerejeshwa kama Mwenyekiti wa Kamati hiyo akiwa na rekodi ya maana.

Yanga ile iliyosumbua ikichukua mataji na kufanya vizuri Afrika, kamati hiyo ilikuwa inaongozwa na Gumbo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.

Nyuma ya Gumbo amerejeshwa pia Lucas Mashauri atakayeendelea kuwa makamu ambaye alikuwa na na mwenyekiti wake ikichukua mataji hayo ya ndani tisa kwa misimu mitatu.

Ndani ya kamati hiyo wamo wajumbe sita wakiwemo watu wazito wawili Seif Ahmed ‘Seif Magari’ na swahiba wake, Davis Mosha ambao ni vigogo wa muda mrefu ndani ya timu hiyo.

Mbali na wawili hao wengine ni Pelegrinius Rutayuga,injinia Mustapha Himba, Majid Suleiman wakati sura mpya ikiwa moja ya Omary Kimosa.

Seif Magari amewahi kuongoza kamati kamati hiyo wakati wa utawala wa Marehemu Yusuf Manji kwa mafanikio makubwa, huku Mosha akiwahi kuwa makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga chini ya uongozi wa marehemu Imani Madega.

Taarifa za ndani ambazo Mwanaspoti imezinasa kwa uhakika ni kwamba kamati hiyo tayari ilishaanza kazi kimyakimya ikiwa na mikakati mizito ya kuhakikisha timu hiyo inakwenda kutetea mataji yao ya ndani lakini pia kuhakikisha Yanga inafika mbali katika Ligi ya Mabingwa.

Nusu ya vigogo hao watashuka nchini Ethiopia kuhakikisha wanaendelea ubabe wao baada ya kuwang’oa Vital’O ya Burundi.

YATUA KWA MAKUNDI

Yanga itatua nchini Ethiopia kwa makundi tofauti ambapo hapa unavyosoma Mwanaspoti kundi la wachezaji waliokuwa nchini Ivory Coast na kikosi cha Taifa Stars limeshatua nchini humo na kupokelewa kisha baadaye kundi la pili ni lile litakalotoka hapa nchini kisha watafuasta kipa Djigui Diarra na kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz KI na mshambuliaji Prince Dube.

Tayari Yanga ilishawatanguliza watu wawili akiwemo Mkurugenzi wa Mashindano, Ibrahim Mohammed Ethiopia kuandaa taratibu zote za awali.

Yanga itashuka uwanjani keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa kuvaana na CBE kabla ya kurudiana nao wiki ijayo na mshindi wa jumla kutinga makundi, Yanga ikitaka kuandika rekodi ya kufika hatua hiyo kwa mara ya pili mfululizo baada ya msimu uliopiota kutinga baada ya miaka 25 kupita na kwenda hadi robo fainali kabla ya kutolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Chanzo: Mwanaspoti