Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yasimamisha mechi Kirumba

Yanga Kirumba Pic Data Yanga yasimamisha mechi Kirumba

Sat, 12 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mechi ya First League kati ya Stand United na Mwadui FC iliyokuwa ianze saa 10:00 jioni imelazimika kusogezwa mbele na kuchelewa kuanza ili kuipisha Yanga ifanye mazoezi yake ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa kesho Novemba dhidi ya Kagera Sugar.

Yanga imefanya mazoezi hayo kuanzia saa 9:15 alasiri katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kuhitimisha saa 10:30 jioni.

Timu hiyo itavaana na Kagera Sugar kesho saa 10 jioni katika Uwanja huo kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa kuanzia saa 10 jioni.

Mchezo huo wa First League ambao Stand United ni mwenyeji ulikuwa uanze saa 10:00 jioni lakini umelazimika kuanza saa 10:43 jioni baada ya Yanga kumaliza mazoezi na programu zake.

Stand United inatumia uwanja wa CCM Kirumba baada ya uwanja wake wa Kambarage, Shinyanga kufungiwa na bodi ya Ligi kutokana na eneo la kuchezea kutokukidhi vigezo.

Mmoja wa wanachama wa Yanga jijini Mwanza ambao wanaongoza msafara wa timu hiyo kutoka na kuingia hotelini wakiwa jijini hapa, Yusuph Budodi ameliambia Mwanaspoti kuwa wameamua kuomba wasimamizi wa mchezo huona wamiliki wa uwanja kwakuwa hakukuwa na eneo lingine la timu yao kufanya mazoezi kwani Uwanja wa Nyamagana kuna mchezo wa Championship kati ya Pamba na Green Warriors.

"Imebidi tufanye 'ujanja' timu ifanye mazoezi kwa kuzungumza na wahusika kwahiyo mchezo ukasogezwa mbele kidogo wakatuambia saa 10:30 jioni tuwe tumamaliza, timu imeanza mazoezi saa 9 na dakika kadhaa hivi," amesema.

Katika mazoezi hayo ya Yanga, kiungo Khalid Aucho amefanya programu za maandalizi ya mchezo wa kesho na wachezaji wenzake huku akionekana kuwa fiti, tofauti na awali ambapo benchi la ufundi lilikuwa linahofia uwepo wake katika mchezo wa kesho.

Chanzo: Mwanaspoti