Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yasimamisha hamasa siku ya mechi ya Simba

Yanga Mashabiki Sdsss.jpeg Yanga yasimamisha hamasa siku ya mechi ya Simba

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema, wanatarajia kufanya hamasa ya nguvu kwa takriban siku tatu na siku ya nne ambayo ni Ijumaa, watawapisha watani zao Simba SC wacheze mechi yao.

Kamwe ameyasema hayo mapema leo Marchi 25, 2024 alipokuwa akielezea mipango yao kuelekea mechi yao dhidi ya Mamelodi Sundowns, mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabigwa Afrika itakayochezwa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

"Tutafanya hamasa ya nguvu kuanzia kesho Jumanne, Jumatano na Alhamisi. Ijumaa tutawaacha wenzetu wacheze echi yao kisha Jumamosi tutakutana Benjamini Mkapa kaushuhudia mechi kubwa Afrika," alisema Kamwe.

Simba wao watakuwa na kibarua cha kuwakabili Al Ahly katika mchezo wao wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika uwanja huohuo wa Benjamini Mkapa jijini Dar siku ya Ijumaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live