Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yashusha kinda mbadala wa Aucho

Djire Abdoulaye Yanga yashusha kinda mbadala wa Aucho

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imeripotiwa kuwa ukingoni kukamilisha dili la kumsajili kiungo mkata umeme kutoka Ivory Coast, Djire Abdoulaye kutoka klabu ya Racing Club Abidjan.

Young Africans SC inahitaji kiungo mwingine mkabaji haraka iwezekanavyo ikiwa ni pendekezo la kocha Miguel Gamondi kwa ajili ya kusaidiana na Khalid Aucho.

Abdoulaye (17) anatazamiwa kukubaliana pia masharti ya kibinafsi na Young Africans licha ya msururu wa vilabu kadhaa vikiwemo ASEC Mimosas na TP Mazembe vinavyowania saini yake.

Yanga SC imewasilisha ofa hivi karibuni ambapo zaidi dola 120,000 (Tsh 299+ million) zinatarajiwa kuwatoka kwa ajili ya kuinasa saini ya kinda huyo anayefananishwa na Mohammed Zougrana ambaye alitimkia MC Algiers baada ya Wananchi kuzidiwa kete.

Kocha wa Young Afticans SC, Miguel Gamondi amependekeza usajili wa kiungo mkabaji ambaye atasaidiana na Khalid Aucho 'The Tank'.

Kikosi bora cha msimu cha Ligi Kuu ya Ivory Coast 21/22 'Ligue 1'

◉ Issa Fofana

◉ Seniko Doua

◉ Attohoula Yao - ASEC

◉ Fabrice Zeguer

◉ Traore Issouf

◉ Abdoulaye Djire

◉ Kipre Tiagouri

◉ Tape Edinho

◉ Karim Konate - ASEC

◉ Stephane Ki Aziz - ASEC

◉ Abdour Kadel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live