Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yashusha chuma kingine

Mpho Muriping Yanga yashusha chuma kingine.

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga haitaki mchezo kabisa, kwani baada ya kutambua mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika sio mchezo, imeamua kushuka mtaalamu mpya kimyakimya.

Wawakilishi wa Tanzania imepangwa Kundi D pamoja na watetezi wa taji hilo, Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria watakaocheza nao Ijumaa ijayo na Medeama ya Ghana.

Mabosi wa Yanga katika kuhakikisha wanamrahisishia kazi Kocha Miguel Gamondi wamemleta mtaalamu wa kusoma mchezo (video Analyst), ili kuliongezea benchi la ufundi la timu hiyo.

Fundi huyo mpya ni Mpho Maruping kutoka Afrika Kusini anayeungana na wataalamu wengine kikosini kujiandaa na vita hiyo ya CAF, Yanga ikianzia ugenini Novemba 24 dhidi ya Waalgeria kabla ya kurudiana na Al Ahly, jijini Dar es Salaam mapema mwezi ujao.

Mtaalam huyo amewahi kufanya kazi na timu ya taifa ya wanawake wa Sauzi ‘Banyana Banyana’ anaijua vyema kazi yake.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema mtaalum huyo kaanza kazi rasmi na yupo kambini.

Katika hatua nyingine mshambuliaji Clement Mzize na Metacha Mnata wameungana na kikosi cha Yanga kambini kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya CRB baada ya kutemwa Stars.

Metacha na Mzize walikuwa sehemu ya wachezaji wa Stars iliyoondoka jana kwenda Morocco na wametua jana jioni mazoeizini Uwanja wa Avic Town Kigamboni.

“Metacha na Mzize wameungana na timu na wamefanya mazoezi na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu Novemba 24 ugenini.” kilisema chanzo hicho kutoka kambi ya Yanga iliyo chini ya Miguel Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: