Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yashitukia umafia wa Magori ishu ya Chama

Chama Mwananchi 01 Yanga yashitukia umafia wa Magori ishu ya Chama

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waswahili Wamenena kwamba biashara asubuhi na jioni mahesabu, ndio kauli waliyoitumia Yanga kukamilisha dili la kiungo Clatous Chama ambaye ametua kwa mabingwa hao na tangu jana ndio gumzo mitandaoni na kwenye vijiwe vya michezo.

Mwamba wa Lusaka Clatous Chama amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga baada ya mkataba wake kumalizika na Simba akigoma kuongeza mwingine sababu kubwa ikitajwa kuwa ni masilahi pamoja na kejeli za hapa na pale.

Mchakato ulikuwa hivi, Simba na Clatous Chama walifanya mazungumzo na Muwekezaji wa Simba Mo Dewji ya kuongeza mkataba mpya, ili aendelea kukipiga Simba lakini Chama alitaja dau kubwa zaidi.

Inaelezwa kwamba Clatous Chama alihitaji Tsh Milioni 820 na mshahara wa Milioni 40 kwa mwezi ndipo asaini mkataba mpya, kwa sababu hiyo biashara ya Chama na Simba iliishia pale.

Sasa upande wa pilli baada ya Clatous Chama kumaliza mkataba wake June 30, Yanga walihisi Simba wanaweza kupindua meza na kumkosa mchezaji huyo ndipo wakamtambulisha haraka.

Lakini Pia Yanga waligundua kwamba endapo Simba watampa Thank You Chama itaharibu biashara yao ya Jezi ingeonekana kama wamesajili mchezaji huru, hivyo kusingekuwa na ukubwa ule kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo inaelezwa na watu wa karibu zaidi na Simba wanasema kwamba, MO Dewji alikuwa analazimisha sana kumbakiza Chama na alikuwa kwenye hatua za mwisho kupindua meza, ndiyo maana Yanga wakamtambulisha Chama bila hata ya kumvalisha jezi ya timu hali iliyozua maswali mengi mitandaoni.

Japo kuna watu wanaamini lolote linaweza kutokea huenda Simba na Chama ndoa yao ikaendelea kadri siku zinavyozidi kwenda, endelea kufuatilia habari za Soka la Bongo ili kufahamu kitakachojili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: