Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yashinda mechi ya mwisho Moro

69004 Khatibu+naheka+picha

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Friends Rangers ya Dar es Salaam, mchezo huo umekuwa maalum kwa kocha mkuu Mwinyi Zahera ambaye alitaka kuwaona baadhi ya wachezaji wake ambao hawakucheza mchezo uliopita dhidi ya Mawenzi Market.

Katika mchezo huo, Yanga ilimaliza dakika 45 za kwanza ikiwa mbele bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Sadney Urikhob akimalizia krosi safi ya kiungo Deus Kaseke dakika ya 44.

Katika kipindi hicho cha kwanza Yanga italazimika kujilaumu yenyewe kufuatia kupoteza nafasi kadhaa kupitia washambuliaji wake Patrick Sibomana na Juma Balinya sambamba na kiungo Mapinduzi Balama.

Friends Rangers ikiongozwa na mshambuliaji wake mtukutu Cosmas Lewis licha ya kujipanga kurudisha bao hilo lakini mashambulizi yao yaliishia katika ukuta wa Yanga.

Kipindi cha pili Yanga ilirudi kwa kasi wakitafuta mabao zaidi lakini umakini ulikuwa mdogo.

Dakika ya 76 kiungo Papy Kabamba Tshishimbi aliipatia Yanga bao la pili kwa shuti kali baada ya mabeki wa Friends kupoteza mpira eneo la hatari.

Mchezo huo umekuwa wa mwisho kwa Yanga katika kambi yao ya Morogoro ambapo timu hiyo itarejea jijini Dar es Salaam Agosti 2 tayari kwa mchezo wa Wiki ya Mwananchi dhidi ya Kariobang ya Kenya.

Chanzo: mwananchi.co.tz