Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yashinda kesi dhidi ya Mzee Magoma

Mama Fatma X Magoma Yanga yashinda kesi dhidi ya Mzee Magoma

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Agosti 9, 2024, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Juma Magoma na wenzake, yaliyolenga kuundoa uongozi wa Klabu ya Yanga madarakani na kuweka kando tuzo na amri zote zilizotolewa katika hukumu iliyowapa ushindi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga, alitoa uamuzi huo wakati wa kusikiliza marejeo ya shauri la maombi namba 187/2022, yaliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga. Katika uamuzi huo, Mahakama imekubaliana na madai ya Bodi hiyo kwamba wazee hao hawakuwa na sifa za kisheria za kufungua shauri hilo.

Zaidi ya hayo, Mahakama imeamuru Magoma, Geofrey Mwaipopo, na Abeid Mohamed Abeid kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hilo kwa Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga. Uamuzi huu unaweka mwisho kwa jaribio la kuondoa uongozi wa klabu hiyo, huku Bodi ya Wadhamini ikipata ushindi katika shauri hilo.

Mzee Magoma na wenzake walishinda kesi waliyokuwa wamefungua mahakamni hapo wakipinga uhalali wa Baraza la Wadhamini la Yanga.

Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama wa Simba, Wakili Simon Patrick amesema; “Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubaliana na hoja nne kati ya tatu ambazo Klabu ya Yanga tulizileta ili zifanyiwe marejeo.

“Kwanza mahakama ya Kisutu imekiri kwamba ni kweli haikuwa na mamlaka na kusikiliza hili shauri. Kwa mujibu wa sheria namba 318 ya mwaka 2002, masuala yote yanayohusu uhalali wa Baraza la Wadhamini yanasikiliza na Mahakama Kuu ya Tanzania.

“Kesi ya akina Magoma ililetwa hapa na ikasikilizwa na mahakama ya Kisutu, hilo lilikuwa kosa la kisheria na kupelekea mahakama ya Kisutu kukubaliana na hoja ya kwanza na kuipiga chini hukumu ya mwanzo.

“Hoja ya pili ambayo imekataliwa na mahakama ya Kisutu ni ile ya kwamba Magoma hakuwa mwanachama halali wakati akifungua shauri hilo. Mahakama imesema suala la uhalali wa uanachama linahitaji ushahidi, kwa hiyo haitasikilizwa.

“Hoja ya tatu ambayo imekubaliwa ni kwamba Mama fatuma Karume (Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Yanga) na mzee Jabiri Katundu kwa njia za ujanja ujanja walinyimwa nafasi ya kusikilizwa.

“Watu walijitokeza mahakamani kuwawakilisha mama Karume na mzee Katundu, mahakama imechunguza kwenye rekodi na kujiridhisha kuwa watu hao hawakuwa na mamlaka kisheria kuwawakilisha mama Karume na Katundu na kupelekea mahakama kuifutilia mbali hiyo hukumu.

“Hoja ya nne ni technique kidogo, hawa watu walileta mamombi yao kwa njia ya petition wakati yalitakiwa yaletwe kama plaint, kwa kuzingatia hoja hizo mahakama ikajiridhisha na kulifutilia mbali shauri hilo.

“Hukumu hiyo imefuta na kwa vile Yanga imetumia gharama kuja hapa mahakamani, kutafuta wanasheria wa kutuaidia, mimi mwenyewe natakiwa nilipwe, nilikuwa na mawakili wengine wa Yanga, mama Karume alikuwa na wakili wake, mzee Katundu alikuwa na wakili wake, hivyo Mzee Magoma na wenzake wamemariwa kutulipa gharama za usumbufu ambazo tukikaa tukapiga hesabu vizuri zitakuwa kama tsh milioni 70 mpaka sh milioni 100," amesema Wakili Simon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live