Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yasaka pointi tatu Sumbawanga

D51e9c0fd5ac7b97fefff159751e95ca.png Yanga yasaka pointi tatu Sumbawanga

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

YANGA imepania kuendeleza wimbi la ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakati leo itakaoposhuka dimbani Sumbawanga kumenyana na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

Yanga wanaongoza ligi wakiwa na pointi 43, wanaingia kwenye mchezo huo wa kwanza wa mzunguko wa pili wakihitaji kuendelea kulinda rekodi wanayoshikilia ya kutopoteza mchezo katika mzunguko wa kwanza.

Wanakutana na Tanzania Prisons, wanaoshika nafasi ya 11 wakiwa na pointi 21 wanaohitaji ushindi kurudisha ari, kwani mzunguko wa kwanza hawakuwa bora sehemu ya ushambuliaji.

Yanga wanaonekana kupewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kwani wachezaji wake wana ari kubwa baada ya kushinda michezo mitano mfululizo, huku Wajelajela wakifanya vibaya mechi nne zilizopita.

Mfano mchezo uliopita, Yanga walicho-moza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ihefu FC, wakati Prisons walipoteza kwa kufungwa 2-0 dhidi ya Biashara United.

Pamoja na rekodi kuonekana zinawapa Yanga nafasi kubwa kuchomoza na ushindi, bado mchezo huo ni vigumu kubashiri matokeo kwani rekodi ya mechi ya mzunguko wa kwanza, wawili hao walitoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kuelekea kwenye mchezo huo kocha wa Yanga Cedric Kaze ametamba wachezaji wake wameandaliwa vyema na wanaingia uwanjani kutafuta ushindi bila kujali wapo ugenini.

Michezo mingine miwili inayotarajiwa kuchezwa leo, Polisi Tanzania watawaalika Azam FC kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro wakati Coastal Union watapepetana na Namungo FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Chanzo: habarileo.co.tz